Jumamosi, 20 Januari 2018

USHAIRI WA KISWAHILI

Ushairi


Ushairi ni utungo wa kisanaa unaotumia lugha teule na mpangilio fulani wa maneno badala ya kutumia lugha natharia(mflulizo).

Ushairi unaweza kuwa kipera cha fasihi simulizi (nyimbo) na pia katika fasihi andishi kwa sababu mashairi yanaweza kuwasilishwa kwa njia ya kukariri na pia kwa njia ya maandishi. Mashairi yanayoghanwa badala ya kuimbwa huitwa maghani.

Uchambuzi

Katika ushairi, tutaangalia:

Istilahi za Kishairi

Haya ni baadhi ya maneno ambayo hautakosa kukutana nayo unapozingatia ushairi. Ni muhimu mwanafunzi kuyajua vizuri.
  • Shairi - ni sanaa ya maneno (utunzi maalum wa lugha ya kisanaa) unaotumia mpangilio na uteuzi maalum wa maneno na sauti ili kupitisha ujumbe fulani.
  • Vina - ni silabi za mwisho katika kila kipande.
  • Mizani - ni idadi ya silabi katika kila mshororo.
  • Mshororo - ni msitari mmoja wa maneno katika shairi.
  • Ubeti - ni kifungu cha mishororo kadhaa.
  • Vipande - ni visehemu vya mshororo vilivyogawanywa kwa alama ya kituo(,)
  • Ukwapi- kipande cha kwanza katika mshororo
  • Mwandamo - Kipande cha tatu katika mshororo
  • Ukingo - kipande cha nne katika mshororo
  • Utao - kipande cha pili katika mshororo
  • Mwanzo - mshororo wa kwanza katika ubeti
  • Mloto - mshororo wa pili katika ubeti
  • Kimalizio/Kiishio - mshororo wa mwisho katika ubeti usiorudiwarudiwa katika kila ubeti.

Ijumaa, 19 Januari 2018

MAIGIZO YA KISWAHILI

Maigizo MAIGIZO Utanzu wa Fasihi Simulizi Vipera vya Maigizo Michezo ya Kuigiza Miviga Ngomezi Malumbano ya Utani Ulumbi Soga Vichekesho Maonyesho ya Sanaa Prev Nyimbo Next Tungo Fupi Maigizo ni sanaa katika fasihi simulizi ambayo watendaji huwa ndio wahusika. 

Maigizo hayasimuliwi kama mbinu nyingine za fasihi. Wahusika ndio huzungumza katika sehemu zao mbalimbali. Mifano: Michezo ya Kuigiza (Jukwaani) - Haya ni maigizo ya jukwaani ambapo watendaji huiga maneno na matendo ya wahusika mbele ya hadhira. Miviga - Miviga ni sherehe mbalimbali katika jamii fulani. Watu hujumukika na sherehe hizi kulingana na tamaduni zao Ngomezi - ni sanaa ya ngoma. Midundo mbalimbali ya ngoma hutumika kuwasilisha ujumbe mbalimbali. 

Malumbano ya Utani - Malumbano ya utani ni mashindano ya kuongea jukwaani baina ya watu wa makundi au jamii mbili ambayo hutumia kejeli na chuku kukejeli tabia mbaya katika jamii au kundi fulani Ulumbi - Ulumbi ni uwezo wa kipekee wa kuzungumza mbele ya hadhira. Mtu mwenye uwezo huo wa kipekee wa kuzungumza jukwaani huitwa mlumbi. Soga - Soga ni mazungumzo baina ya watu wawili au zaidi ambayo aghalabu huwa hayana mada maalum. Vichekesho - Vichekesho ni aina ya sanaa ya fasihi simulizi ambayo watu hutoa vihadithi vifupi au sentensi zenye uwezo wa kuwafanya wasikilizaji wacheke. 

Maonyesho ya Sanaa - Maonyesho huhusisha watu wa jamii au kundi fulani wanaoonyesha taaluma, ujuzi au sanaa yao kwa watazamaji. Comments Login to Comment 16 comments. Hide Reported Comments Muzammil Sayani • Aug 12, 2017 Je, Sifa Za Maigizo ni nini? Reply Like 0 likes Victor • Jun 21, 2015 Soga ni mazungumzo ya kupitisha wakati na lugha utumiwayo si rasmi ilhali ulumbi ni uhodhari wa kuzungumza kwa ufasaha na madoido Reply Like 0 likes james nganga • Jun 09, 2015 matumizi ya methali maigizo nyimbo na vitendawili katika kusuruhisha migogoro Reply Like 0 likes lovejoy victoria • May 17, 2015

 Je,ni nini tofauti kati ya ulumbi na soga. Reply Like 0 likes edmard murimi • Nov 05, 2017 rejelea apo awali Reply Like 0 likes Ngige Benson • Mar 18, 2015 Swali: strawberry kwa kiswahili ni nini? Reply Like 0 likes Jared Ekirapa • Jul 10, 2014 1.Je,nzige au panzi ana macho mangapi? 2.Neno 'particle' ni nini katika lugha ya kiswahili? 3.Ni nani huangua vifaranga vya kuku? Reply Like 0 likes Jared Ekirapa • Jul 10, 2014 Jibu swali hili na ueleze kama ni fumbo au chemsha bongo; Nilitaka kununua sukari ambayo ilikuwa shilingi 97 na sikuwa nazo. Ilinibidi kukopa pesa kwa mama yangu shilingi 50 na pia nikakopa baba yangu shilingi 50 ili nikanunue sukari.

Kwa hivyo nilikuwa na deni la mama shilingi 50 na baba pia shilingi 50.Nilinunua sukari na nikarudishiwa shilingi 3 kutoka kwa duka.Kwa hizo pesa shilingi 3,nilimpa mama shilingi 1 na baba pia shilingi 1 ili nikapunguze madeni niliyokuwa nayo na nikabaki na shilingi moja.Kumbuka kuwa deni la mama ni 49 na baba pia ni 49 na 49+49=98,98 ukiongeza shilingi 1 niliyokuwa nayo ni 99 yaani 98+1=99.Je,shilingi 1 ilienda wapi ili iwe 100? Ukishindwa kulijibu au ukitaka kunijibu wasilisha kwa; jaredekirepa@yahoo.com,pia iwapo unahitaji mafumbo au chemshabongo zaidi utapata bila wasiwasi. Reply Like 0 likes DUNCAN IRUNGU. • Mar 05, 2014 Unyago ni tendo la kuwapasha wasichana tohara. Reply Like 0 likes Issack malela • Jul 26, 2013 Unyago ni nini? Reply Like 0 likes Silah Rokito Chelimo • May 09, 2013 Mtunzi wa nyi